Gospel Global Bahati Bukuku – Lazima Usamehe

Bahati Bukuku – Lazima Usamehe

Download Lazima Usamehe Mp3 by

Here's a song by the African prolific music artist and talented singer ““. This song is titled “Lazima Usamehe”, as it was released alongside its video. You'll also be blessed.

Download Audio Mp3, Stream, Share, and stay graced

DOWNLOAD HERE

DOWNLOAD MORE BAHATI BUKUKU SONGS HERE

Lyrics: Lazima Usamehe by

Wewe, wewe, wewe
Unasema huwezi, huwezi, huwezi
Huwezi
Naomba niseme yaliyonikuta
Naomba niseme niliyoyaona
Naomba niseme yaliyonikuta
Naomba niseme niliyoyaona
Nilikua na rafiki yangu mzuri
Aliyeumua ugonjwa wa ajabu
Kwa huruma zangu nikamhurumia
Nikatumia muda wangu mwingi
Nikazunguka huku na kule kutafuta madaktari
Nikatembea huku na huko kutafuta uzima wake
Lakini Mungu sio mwanadamu alinihurumia
Akaachilia uzima moyoni mwake akawa mzima
Nikatafuta ata wachungaji nao walimuombea
Nikatafuta ata wana maombi wakamuombea
Lakini Mungu sio mwanadamu alinisikia
Niliposema Mungu mponye, alinisikia
Kwa kuwa Mungu sio mwanadamu alimponya
Cha kushangaza alipopona, malipo yangu
Cha kushangaza alipopona, malipo yangu
Amegeuka adui yangu, mimi mwenzenu
Amekuwa msiba kwangu, mimi mwenzenu
Nasema siwezi, siwezi
Siwezi, siwezi
Siwezi kumsamehe huyu
Siwezi kumsamehe huyu
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Naomba niseme yaliyonikuta, mimi mwenzenu
Naomba niseme yaliyonifika, mimi mwenzenu
Kama wema ni uadui, basi umenifika
Kama wema ni uadui, basi ni zamu yangu
Ameleta msiba, huyo
Ameuwa watoto wangu, mimi mwenzenu
Ameleta kilio, huyo
Amevunja na ndoa yangu, mimi mwenzenu
Nasema siwezi, siwezi
Siwezi, siwezi
Siwezi kumsamehe huyu
Siwezi kumsamehe huyu
Ni kweli umeumizwa wewe
Ni kweli umedharauliwa wewe
Ni kweli umekata tamaa wewe
Unasema huwezi, huwezi
Huwezi, huwezi
Lakini huyo ndio ushindi wako
Analeta heshima ya jina lako
Huyo ndiye ngazi ya kupandia wewe
Ili Mungu akuinue
Lazima ukutane na hayo
Unayo yapitia ili Mungu aseme nawe
Ni lazima adui zako wainuke
Yeye akuinue mbele ya macho yako oh
Mbele ya macho yako oh
Ili Mungu akuinue
Ni lazima adui zako wainuke
Ni lazima
Ili Mungu akuinue ni lazima watu wapigane nawe
Ili Mungu akuinue ni lazima ushuhuda wako utimie
Ili Mungu akuinue ni lazima awatenge mbali wale adui zako
Ili Mungu akuinue ni lazima apepete makapi kwanza
Ili wale wasiofaa ni lazima watajitenga na wewe
Wale ambao ni kusudi lake ni lazima watalia pamoja nawe
Ili Mungu ajitukuze ni lazima upitie majaribu hayo
Ili Mungu akuinue, ni lazima ata ndugu wajitenge nawe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Lazima usamehe ili Mungu akuinue
Lazima usamehe ili Mungu aseme nawewe
Nilazima ili Mungu akuinue
Nilazima

Comment below with your feedback and thoughts on this post.